Kikosi chetu kimeondoka asubuhi kuelekea jijini Arusha tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Alhamisi, Oktoba 29 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.
Kikosi kimeondoka na wachezaji wote baada ya kukamilisha mpango wa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga jumla ya mabao 9-1 FC 15 De Agosto kutoka Equatorial Guinea.
Timu itakuwa Arusha kwa siku mbili kwa ajili ya programu ya mazoezi kabla ya kuelekea Manyara kutokana na uhaba wa Viwanja.
Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna aliyepata maumivu kwenye mchezo wa jana dhidi ya 15 De Agosto kitu ambacho kinamfanya kocha mkuu Steve Barker kuwa machanguo mengi.