Tumefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja Uhuru Dar es Salaam.
Anicet Oura alitupatia bao la kwanza dakika ya tatu kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Elie Mpanzu kufuatia kona iliopigwa na Nathaniel Chilambo.
Raimond Luulendi aliipatia Namungo bao la kusawazisha dakika ya 35 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Rashid Chambo.
Lulendi aliipatia Namungo bao la pili dakika ya 43 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Chambo.
Rushine De Reuck alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 79 kwa mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji Ibrahim Doumbia kufanyiwa madhambi na mlinzi Rogers Gabriel ndani ya 18.
Oura alitupatia bao la tatu dakika ya 89 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mpanzu.
Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 30 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kushinda mechi zote 10.
X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Nindi (Morice 45'), De Reuck, Kagoma, Gueye (Makgalwa 63')Maema, Mpanzu (Jabaar 90+3'), Chama (Doumbia 73') Oura
Walioonyeshwa kadi: Chilambo 90+6'
X1: Seleman, Jigwa, Hance, Okechi, Kaniki, Nyenye, Lukindo (Alobogast 86'), Kapama, Raymond, Dunia (Kikoti 90+5'), Chambo (Makang'a 90+5')
Walioonyeshwa kadi: Jigwa 18' Lulendi 46+3' Kapama 63' Okechi 68'