Simba Sports Club

Timu yafanya Mazoezi ya mwisho Uwanja wa Arusha

28 Oct 2026

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Shule ya Costantine jijini Arusha tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Tanzanite Kwaraa saa 10 jioni.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunataka kupata alama tatu muhimu ugenini.

Advertisement

Morali za wachezaji zipo juu na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo ingawa tunajua utakuwa mgumu kutokana nakuwa tunacheza ugenini.